Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa katika mgogoro na vituo vya runinga nchini humo akisema kuwa baadhi ya vituo vimekuwa na upendeleo huku akionya kwamba atafutilia mbali leseni zao.

Trump alikasirishwa na ripoti ya kituo cha habari cha NBC iliyodai kwamba aliwaagiza maafisa wake wa usalama na majenerali kuongeza kiwango kikubwa cha silaha za kinyuklia nchini humo, Trump alisema kuwa habari hiyo ilitungwa.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis naye pia aliitaja taarifa hiyo iliyotolewa na kituo cha NBC kama habari isiokuwa ya ukweli.

Wiki iliopita NBC iliripoti kwamba waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson alimuita rais Trump ‘mtu mjinga’ matamshi ambayo Tillerson hajayapinga lakini rais Trump ameyataja kuwa habari bandia.

Wanahabari nchini Marekani wanasema kuwa rais huyo atapata shida kufuta leseni za vyonbo vya habari,  kwa kuwa zinadhibitiwa na tume ya mawasiliano nchini humo huku pia baadhi ya makundi ya kupigania haki yanasema kuwa rais Trump anaweka mfano mbaya kwa viongozi wengine.

Australia yadukuliwa siri za kijeshi
Video: Sheikh Ponda ajitosa rasmi tukio la Lissu, Rais Magufuli, Aga Khan wazungumzia mambo 3