Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kuhutubia viongozi kutoka nchi 40 za Kiislam ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kwanza kufanyika katika nchi za kiarabu ambapo atatoa hotuba hiyo akiwa nchini Saudi Arabia.

Katika hotuba yake hiyo nchini Saudi Arabia, anatarajiwa kutoa wito wa pamoja wa kukabiliana na imani ya kiitikadi kali ambayo imeonekana kuwa tishio kwa usalama wa raia hasa inapokea migogoro.

Aidha, Trump ameanza ziara yake leo kwa kufanya mikutano na baadhi ya marais akiwemo Abdul Fatal el Sisi wa Misri na Mfalme wa Bahrain ambapo faihda ya mkutano huo inategemea na namna atakavyozungumza na kilichomo kwenye hotuba yake.

Hata hivyo, hatua yake ya hivi karibuni ya kupiga marufuku safari ya kwenda Marekani kwa raia wa mataifa 7 yenye waislamu wengi duniani, ilisababisha hasira kote katika mataifa ya kiislamu.

Wakulima wa karafuu kunufaika na mkopo
Serengeti boys kupambana na Niger leo