Marais kutoka nchi mbalimbali za Ulaya na America wamelaani shambulio la kigaidi lililotokea jana usiku katika daraja la London nchini Uingereza lililoua watu 7 na wengine 48 kujeruhiwa katika shambulio hilo.

Rais wa Marekani, Donald Trump katika ukurasa wake wa tweet amesema kuwa,”Marekani iko tayari kusaidia Uingereza kwa chochote kile kwani ugaidi haukubariki duniani na sehemu yeyote kwa sababu unaangamiza maisha ya watu wasiokuwa na hatia.

Aidha, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron katika ukurasa wake wa tweet naye akaandika “Ufaransa iko bega kwa bega na Uingereza katika kusimamia amani baada ya mashambuli hayo.

Naye Bi Angel Merkel wa Ujerumani akasema kuwa “Ulaya inaungana na Uingereza kupambana na vitendo vya ugaidi kwani vinahatarisha maisha ya watu wasiokuwa na hatia katika jamii.

Hata hivyo, nchi nyingi za umoja wa Ulaya na America zimelaani tukio hilo la kigaidi na kuahidi kuungana na Uingereza kupambana na washambuliaji hao kwani wanahatarisha amani.

Fainali ya UEFA yasababisha mashabiki 1000 wa mpira kujeruhiwa
Ronaldo aonyesha ubora wake UEFA