Baada ya kuibuka kuwa mshindi, Trump amezungumza na wananchi wa Marekani mjini New York ambapo ametumia nafasi hiyo kuwashukuru kwa kumchagua kuwa rais wao baada ya Barack Obama kumaliza muda wake.

Trump amesema atatumia muda wake kuwatumia Wamarekani na katika kipindi ambacho atakuwa madarakani atahakikisha kila Mmarekani anajivunia uwepo wake na kuwataka kushirikiana nae kwani yeye ni rais wa Wamarekani wote.

“Nitakuwa rais wa Wamarekani , na hilo ndilo jambo muhimu kwangu, sitawaangusha nitafanya kazi, kwakuwa uchaguzi umemalizika ni muda sasa wa kazi kuanza na baada ya miaka miwili au mitatu au hata minane kila mmoja atakuwa anajivunia uwepo wangu,”amesema Trump.

Maofisa Wa TFF Wapandishwa Kizimbani Kwa Tuhuma Za Rushwa
Bale ashinda tuzo ya mchezaji bora Wales