Mgombea Urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican, Donald Trump amelitolea jicho la shari ya dunia nzima tukio la kigaidi lilifanywa hivi karibuni katika mji wa Nice nchini Ufaransa ambapo mtu mmoja alifyatua risasi na kuua watu 84 katika sherehe za ‘Bastille Day’.

Akizungumza katika mahojiano na mtangazaji wa Fox News, Trump aliendelea kuelekeza lawama zake kwa kundi la kigaidi linalojiita Islamic State (IS) pamoja na wahamiaji wenye imani ya dini ya kiislamu akidai kuwa ndio chanzo cha matukio hayo.

Trump alisema kuwa kama angekuwa Rais wa Marekani, ulikuwa muda muafaka kwake kutangaza vita ya dunia kwakuwa nchi inashambuliwa kutoka pande mbalimbali za dunia kama ilivyokuwa kwa vita ya pili ya dunia. Alisema kuwa tofauti kati ya vita hizo ni kwamba hivi sasa washambuliaji hawana sare zinazowatambulisha.

Amesema kuwa angeliomba Bunge la Marekani (congress) kupitisha tangazo rasmi la vita ya dunia hususan kutokana na mashambuzi kama hayo ambayo yalilikumba taifa hilo mwaka huu.

“Kama unaiangalia hii, hii ni vita, inayokuja kutoka sehemu tofautitofauti. Na kwakweli, ni vita ambayo tunapambana na watu hawana sare. Unajua, zamani kungekuwa na sare hivyo ungejua unapambana na nani,” alisema Trump.

Alikosoa vikali sera za mgombea na hasimu wake wa kisiasa, Hillary Clinton wa chama cha Democratic za kuwaruhusu wahamiaji kuingia nchini humo bila kuwabagua.

“Hawa watu tunawaruhusu kuingia nchini bila kufahamu wanatoka wapi, ni kina nani, hawana kumbukumbu zao za maandishi, hawana nyaraka mara nyingi. Halafu Hillary Clinton anataka kuwaruhusu wengi zaidi hata ya alivyofanya Obama,” Trump ananukuliwa.

BASATA yaufungia wimbo wa Nay wa Mitego ‘Pale Kati Patamu’
Aliyeoongoza kidato cha 6 ni tunda la Shule ya Kata, aeleza alivyodharauliwa