Watu maarufu Duniani wameonesha kuumizwa na kifo cha mchezaji kobe, miongoni mwa watu hao ni Rais wa Marekani Donald Trump na Rais mstaafu wa marekani Barrack Obama ambapo wameonesha masikitiko yao kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Kupitia ukura wa tweeter wa Rais Trump ameandika kuwa “Kobe Bryant ukiachilia mbali kuwa alikuwa Mchezaji mzuri wa Basketball wa wakati wote, alikuwa ndio anaanza kuyaishi Maisha, aliipenda familia yake sana, kifo cha mwanae Gianna kinaumiza zaidi, mimi na mke wangu tunampa pole mkewe Vanessa na wote walioguswa na kifo hicho”

Naye Barrack Obama ameandika kuwa “Kobe alikuwa ni Legend, maombi yetu kwa Vanessa na Familia, kumpoteza Binti mdogo Gianna Bryant ni maumivu zaidi kwetu kama Wazazi”

Shaquille O’Neal,ambaye alicheza na Bryant huko Lakers kati ya mwaka 1996 na 2004, amesema kuwa hana neno la kusema kwa sababu ya maumivu.

“Ninakupenda na utakumbukwa,” ameandika katika mtandao wa Instagram wakiwa katika picha ya pamoja na jezi zao za Lakers.

Mwanamuziki Kanye West ameandika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twitter kuwa Bryant aliishi maisha ambayo yaliwavutia wengi.

Wengine ni wachezaji wenzake wa Basketball pamoja na  wachezaji wa mpira wa miguu wakiwemo Ronaldo, Messi, Pogba na wengine wamemlilia kupitia mitandao ya kijamii.

China kujenga hospitali ya wagonjwa wa Corona ndani ya siku sita
Chama tawala Burundi kimemtangaza mrithi wa Nkurunziza

Comments

comments