Rais wa Urusi, Vladimir Putin anatarajiwa kukutana na rais wa Marekani, Donald Trump baada ya Trump kutishia kuwa Marekani itajiondoa katika mkataba wa kudhibiti silaha za nyuklia kati ya Urusi na Marekani, INF.

Kufuatia kitisho hicho cha Marekiani kujiondoa katika mkataba wa kudhibiti silaha za nyuklia kati ya nchi hizo (INF), Rais Putin amesema kuwa anataka kukutana na rais wa Marekani Donald Trump kwa mazungumzo mjini Paris.

Aidha, tangazo la kushtukiza la Trump kujiondoa katika mkataba huo limesababisha hisia mbali mbali kutoka kwa viongozi wa mataifa ya Ulaya.

Katika mkutano wake na mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa Marekani, John Bolton jijini Moscow, Putin amesema kuwa yuko tayari kukutana na Trump hivi Karibuni.

Hata hivyo, marais hao wanatarajiwa kuonana tarehe 11 Novemba pembezoni mwa sherehe za kuadhimisha miaka 100 ya kumalizika kwa vita vya kwanza vya dunia.

Trump avalia njuga mauaji ya mwandishi Saudi Arabia
Upasuaji wa Hawa wamalizaka, madaktari wamtabiria haya