Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa hatofanya kazi na chama pinzani nchini humo cha Democratics kwa jambo lolote lile mpaka pale uchunguzi dhidi yake utakapo kamilika.

Vita ya maneno ilizuka jijini Washington kati ya Rais, Donald Trump na Spika wa Baraza la Wawakilishi’ Nancy Pelosi kutokana na kuongezeka kwa uchunguzi unaofanywa na wabunge kwamba Trump alihusika katika kuficha ukweli wa mambo katika uchaguzi mkuu uliopita.

Trump anayetarajia kugombea katika uchaguzi mkuu wa Rais nchini humo mwaka 2020 kupitia chama tawala cha Republican amesema kuwa hatofanyakazi na wa-Demokrats juu ya masuala ya kukarabati miundo mbinu au jambo jingine lolote hadi uchunguzi unaofanywa juu yake unamalizika.

Aidha. Trump na Wademokrats wanaodhibiti baraza la wawakilishi la bunge wako katika mvutano mkali wa kupigania madaraka juu ya uwezo wa wabunge kumchunguza rais baada ya kumalizika kwa uchunguzi wa Mueller juu ya ikiwa Russia iliingilia kati uchaguzi wa Marekani 2016.

Trump amesema kuwa hawezi kufanya kazi na Wademokrats katika mazingira kama hayo, hivyo anawataka kuacha kabisa uchunguzi huo aliouita wa uongo.

Muda mfupi baadaye mkuu wa wachache katika baraza la Seneta, Chuck Schumer alimshutumu rais kwa kupanga kwa makusudi tukio la Jumatano kama kisababu cha kukwepa majadiliano.

Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya mvutano huo kwa upande mmoja ni kichekesho lakini wakati huo huo ni tukio muhimu ambalo halifahamiki lita athiri vipi kazi za vyombo hivyo viwili vya utawala.

Rais Putin apata watoto Mapacha
Hukumu ya Masele yawekwa hadharani

Comments

comments