Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa mkutano wake na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un unatarajiwa kutafanyika baadaye mwezi huu, kwenye mji mkuu wa Vietnam, Hanoi.

Trump ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba wawakilishi wake wameondoka Korea Kaskazini baada ya kufanya mazungumzo yaliyofanikiwa na wamekubaliana kuhusu muda na siku ya kufanyika kwa mkutano huo wa kilele kati yake na Kim.

Amesema kuwa mkutano huo wa pili kati ya viongozi hao utafanyika Februari 27 na 28. ambapo Trump na Kim walishawahi kukutana kwa mara ya kwanza mwaka uliopita huko Singapore.

Aidha, Trump amebainisha kuwa Korea Kaskazini chini ya uongozi wa Kim, itakuwa nchi yenye uchumi mkubwa zaidi duniani hivyo amesema kuwa amejiandaa kukutana na Kim ili kuendeleza mchakato wa amani.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema kuwa mjumbe maalum wa Marekani nchini Korea Kaskazini, Stephen Biegun atakutana tena na maafisa wa Korea Kaskazini kabla ya mkutano wa Trump na Kim. Biegun amewasili Seoul, Korea Kusini akitokea Pyongyang baada ya kufanya ziara ya siku tatu ambako alijadiliana na maafisa wa Korea Kaskazini kuhusu mkutano wa viongozi hao.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imesema kuwa Biegun alijadiliana kuhusu nia ya Kim kuachana na silaha za nyuklia, kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Korea Kaskazini pamoja na kuweka amani ya kudumu katika Rasi ya Korea.

 

Mtoto atangaza kuwaburuza mahakamani wazazi wake
CCM kuwatosa viongozi wasiowajibika, 'Hatuwezi kuwa na viongozi mizigo'

Comments

comments