Rais wa Marekani, Donald Trump anatarajia kukutana na rais wa Urusi, Vladmir Putin kwa mara ya kwanza nchini Ujerumani, wakati wa kushiriki kikao cha G20.

Marais hao wa nchi mbili hasimu zenye nguvu wanatarajia kufanya mkutano wao binafsi kuzungumzia majeraha ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili yaliyotokana na migogoro ya Syria na Ukraine, pamoja na sakata la Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani.

Kambi ya mpinzani wa Trump kwenye uchaguzi wa Marekani, Hillary Clinton imeendelea kushikilia msimamo wake kuwa Urusi iliingilia uchaguzi na kubadili matokeo halisi katika majimbo muhimu.

Nchi za G20 zinakutana nchini Ujerumani kuzungumzia masuala mbalimbali likiwemo suala la mabadiliko ya tabia nchi na biashara za kimataifa kati yao.

G20 ni kundi linalojumuisha nchi 19 zilizoendelea na zinazoendelea pamoja na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kukamilisha 20.

Nchi hizo ni pamoja na Argentina, Australia, Brazil, Canada, China, Ufaransa, Ujerumani, India, Indonesia, Italia, Japan, Mexico, Urusi Saudi Arabia, Afrika Kusini, Korea Kusini, Uturuki, Marekani na Uingereza.

Utafiti WHO: Mtindo huu wa kufanya mapenzi unawapoteza mamilioni duniani
Video: Kimewaka tena Kibiti, Jaji wa Escrow ajiuzulu