Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema wapo tayari kwa mchezo wa Ngao wa Jamii utakaopigwa Kesho Jumamosi (Agosti 13) Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba SC yenye Kiu ya Mataji baada ya kuyapoteza Msimu uliopita itakutana na Young Africans kwenye mchezo huo, huku ikiwa na deni la kupoteza kwa 1-0, dhidi ya Young Africans mara mbili.

Try Again amesema dhamira yao kubwa ni kuhakikisha wanacheza vizuri katika mchezo wa Kesho na Kushinda, ili kuwapa furaha Mashabiki na Wanachama wa Simba SC ambao walimaliza Msimu uliopitakwa majonzi.

“Msimu uliopita tulipoteza mchezo wetu wa ufunguzi na wao, ilikuwa sehemu ya mchezo tukajikuta tunapoteza mataji yetu yote,” alisema Try Again na kuongeza:

“Kwa sasa tumedhamilia haswa kuanzia Jumamosi kuyarejesha mataji yetu tuliyotamba nayo misimu minne mfululizo, kikosi tunacho na ndio maana tumetoa mtu tukaweza mtu.”

Simba SC ilipoteza kwa 1-0 katika mchezo wa Ngao ya Jamii Msimu uliopita, bao la Young Africans likifungwa na Mshambuliaji kutoka DR Congo Fiston Kalala Mayele.

Matokeo kama hayo yaliikuta tena Simba SC kwenye mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, bao likifungwa na Kiungo Mshambuliaji wa Young Africans Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Katika michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu uliopita ‘2021/22’ Miamba hiyo ya Kariakoo-Dar es salaam ilishindwa kufungana kwa kuamblia matokeo ya sare (0-0).

Kenya: IEBC yapongezwa kwa usimamizi zoezi la kura
Kenya: Wanahabari kujadili utoaji matokeo kwa kutofautiana