Baada ya kukamilisha mchezo wa kiporo dhidi ya Azam FC Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wanatarajiwa kuondoka nchini kuelekea DR Congo kwa ajili ya majukumu ya Kimataifa, ambapo Ijumaa (Februari 12) watakuwa dimbani kuwakabili wenyeji wao AS Vita Club.

Simba SC itaondoka nchini kesho Jumanne (Februari 09) ikiwa na kikosi chake kamili kwa ajili ya mchezo huo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema wataondoka na wachezaji wote waliowasajili kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa.

Try Again amesema kutokana na uwepo wa janga la Corona, watawachukua wachezaji wote kwa ajili ya tahadhari, kwa sababu wanafahamu kikosi chao kitafanyiwa vipimo vya Corona kabla ya mchezo huo.

“Endapo itabainika mchezaji yetu yoyote atakutwa na maambukizi, tunajua tutakua na hazina ya kutosha kwa kumuwezesha kocha Gomez amtumie nani kwenye mchezo huo ambao tunauchukulia kwa umuhimu mkubwa sana.”

“Soka la Afrika linazunguukwa na mambo mengi, tunajua hujuma za wapinzani hasa katika kipindi hiki ambacho Corona inaweza kutumika kutudhohofisha, hivyo tumeamua kujipanga kwa kupeleka wachezaji wote DR Congo.” Amesema Try Again.

Wakati huo huo Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema mchezo dhidi ya Azam FC umemsaidia kufanya maboresho muhimu ya kikosi chake kabla ya kuwakabili AS Vita Club siku ya Ijumaa. Simba SC imepangw akundi A sambamba na mabingwa watetezi Al Ahlyya Misri, AS Vita Club ya DR Congo na Al Mereikh ya Sudan.

Ebola yaibuka tena Congo
Waziri Kalemani awasimamisha vigogo Tanesco