Beki wa kushoto wa vinara wa ligi kuu ya soka Tanzania bara (Simba SC), Mohamed Hussein Zimbwe Jr huenda akajiunga na miamba ya soka nchini Kenya Gor Mahia, baada ya kocha wa timu hiyo Muingereza Dylan Kerr, kuonyesha kuvutiwa na kiwango cha nahodha huyo msaidizi wa kiosi cha Joseph Omog.

Zimbwe Jr au Tshabalala amesema kama inatokea nafasi hiyo yupo tayari kwa sababu Gor Mahia ni klabu kubwa Afrika Mashariki na ni furaha kubwa miongoni mwa wachezaji wa kigeni wanaochezea timu hiyo yenye historia na mafanikio makubwa nchini humo.

“Kwa nini nikatae kwa sababu mpira ndiyo kazi yangu na Gor Mahia ni timu kubwa yenye hadhi kama ya Simba, kwa hiyo sioni sababu ya kugoma zaidi nitafurahi kwasababu nitakwenda kujiongezea ujuzi kwa kukutana na changamoto mpya kwenye ligi nyingine,” amesema Tshabalala.

Beki huyo ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi ya Vodacom msimu uliopita amesema bado hajapata taarifa yoyote ya yeye kutakiwa na mabingwa hao wa Kenya, lakini endapo itazipata taarifa mapema atahakikisha anakwenda Nairobi kwa ajili ya kukamilisha mazungumzo na taratibu nyingine za kujiunga na miamba hao wa kenya.

Kerr amewahi kuifundisha Klabu ya Simba, na kwa bahati mbaya alitimuliwa baada ya mzunguko wa kwanza, kumalizika na nafasi yake kuchukuliwa na Mganda Jackson Mayanja, kocha huyo amekuwa na mapenzi makubwa na wachezaji wa Tanzania na Afrika.

Kafulila atua rasmi CCM
Mwanariadha mlemavu aongezewa kifungo jela