Nahodha msaidizi wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ amesema watapambana kufa na kupona ili kuchukua Kombe La Shirikisho Tanzania Bara (ASFC) na  kudhihirisha kuwa hawakutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa kubahatisha.

Simba itacheza fainali ya ASFC Agosti 02, 2020 dhidi ya Namungo FC katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga.

Kikosi cha timu hiyo kiliondoka jana Jumanne saa sita mchana kwenda Tanga kuikabili Coastal Union kwenye mchezo wa Ligi Kuu utakaofanyika kesho Al-Khamis, kisha kitaelekea Kilimanjaro kumaliza msimu huu kwa kucheza na Polisi Tanzania, halafu Sumbawanga, Rukwa kucheza fainali ya ASFC.

Tshabalala amesema wamejipanga vizuri kwa ajili ya kushinda mchezo huo wa fainali ili kulinda heshima ya Simba na kuonyesha kuwa msimu huu walikuwa bora kila eneo.

Amesema watahakikisha wanashinda michezo miwiwli iliyobaki ya Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union na Polisi Tanzania ili kuivutia kasi Namungo.

Matokeo Majimbo mengine 70 kura za maoni CCM
CRDB Marathon kurindima Agosti 16