Nahodha na kiungo wa Young Africans Papy Tshishimbi na winga Beranrd Morrison hawakujumuishwa kwenye kikosi kilichoelekea kanda ya ziwa kwa ajili ya michezo dhidi ya Biashara United na Kagera Sugar.

Tshishimbi alianza mazoezi mapema juma hili. Mcongomani huyo ameachwa aimarike zaidi tayari kuwakabili Simba SC kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la FA, Julai 12.

Morrison alirejeshwa kikosini juzi baada ya mvutano na mabosi wake kufikia tamati. Hata hivyo kocha Luc Eymael alimuondoa mapema tu kwenye kikosi chake ambacho kimewasili Musoma, Mara kwa kuwa hakuwa amefanya mazoezi na timu siku kadhaa nyuma.

Hata hivyo Eymael alisema Morrison anaweza kuungana nao mkoani Kagera kama ataona kuna umuhimu kumtumia mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

Lakini amewahakikishia Wanajangwani kuwa Morrison atakuwa sehemu ya kikosi chake kitakachoikabili Simba Julai 12.

'Top 5' wagombea urais Zanzibar
Simba SC watangaza njaa Mtwara