Kampuni ya TSN  Kwa kushirikiana na Wasanii wa bongo fleva na bongo Movie wamejitokeza kuwezesha mechi maalum kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa wa Kagera.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Biashara wa kampuni hiyo, Jahu Mohamed Kessy ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi Jumapili, Septemba 25 kushuhudia mechi hiyo  itayofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Aidha, Kessy alitoa wito kwa mashirika mengine kujitokeza kwa wingi kushiriki tukio hilo la kuwachangia wahanga wa tetemeko hilo lililotokea mwanzoni mwa mwezi huu.

Alisema kuwa ushiriki wa TSN umetokana na kuguswa na tukio hilo na kwamba wameona ni njia sahihi kuwatumia wasanii wa bongo movies na bongo fleva kufanikisha tukio hilo pamoja na kuwashirikisha wengine wenye mapenzi mema kwa kile walichojaliwa. 

“TSN, Tanzania sisi Nyumbani, tunaunganisha nguvu ya wasanii hawa kutoka katika tasnia hizi mbili tofauti  kwa lengo la kuhamashisha uchangiaji wa pamoja,” alisema.


 Mkuu wa kitengo cha Masoko na Biashara TSN, Jahu Mohammed Kessy akiwakabidhi wasanii jezi kwa ajili ya mechi ya kuchangia maafaa ya tetemeko la ardhi Bukoba

Mechi hiyo inatarajiwa kuanza majira ya saa tisa mchana.

Kamati Ya Katiba, Sheria Kujadili Kesi 13 Kesho
Ligi Daraja La Kwanza Msimu Wa 2016/17 Yaanza