Meneja wa klabu ya Chelsea Thomas Tuchel, amemjibu aliyekuwa meneja wa Inter Milan ya Italia Antonio Conte ambaye juma lililopita alionesha kuchukizwa na mwenendo wa Mshambuliaji Romelu Menama Lukaku Bolingoli.

Conte alionesha kutoridhishwa na mwenendo wa Mshambuliaji huyo tangu alipoarejea Chelsea, kwa kusema benchi la ufundi la klabu hiyo limeshindwa kumtumia ipasavyo na ndio maana kasi yake ufungaji imepungua.

Tuchel kwanza ameanza kwa kuwataka radhi mashabiki wa Inter Milan kwa kile wanachokiona kwa Mshambuliaji huyo, huku akitoa sababu za kuamua kumsajili Lukaku mwezi Agosti mwaka huu.

“Samahani kwa mashabiki wa Inter, lakini tulimtambua yeye kama mchezaji ambaye anaweza kutoa hamasa kubwa kwa wachezaji vijana,” alisema Tuchel.

“Mara zote amesema alikuwa yupo vizuri kule Inter na (Antonio) Conte kwa sababu alifanikiwa kupata matokeo mazuri, lakini kwake yeye ilikuwa ni muhimu kurudi sehemu ambayo aliwahi kucheza wakati akiwa kijana.” amesema Tuchel.

Hadi sasa Lukaku ameshaifungia Chelsea mabao manne katika michezo tisa kwenye mashindano yote msimu huu.

Watu watatu wanashikiliwa Polisi kwa mauaji ya Mtendaji Mbezi
Thomas Tuchel: Jorginho mchezaji bora duniani