Meneja wa klabu ya Borussia Dortmund, Thomas Tuchel amewatumia salamu washika bunduki wa Ashburton Groove (Arsenal) kwa kuwataka wasahau suala la kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang.

Tuchel, ametuma salamu hizo, baada ya taarifa kuibuka na kudai kwamba Arsenal wapo katika mipango ya kutaka kutuma ofa ya paund million 44.6, kwa lengo la kumsajili mchezaji huyo ambaye kwa sasa ndiye bora katika bara la Afrika baada ya kutangazwa mwishoni mwa juma lililopita.

Meneja huyo ambaye alichukua nafasi ya kuwa mkuu wa benchi la ufundi la Borussia Dortmund, baada ya kuondoka kwa Jurgen Klopp mwishoni mwa msimu uliopita, amesema hatarajii na wala hategemei kumuachia Aubameyang kama inavyodhaniwa na walio wengi.

Amesema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, bado ana mkataba wa miaka minne ambao utafikia kikomo mwaka 2020, hivyo kilichomo katika makubaliajno hayo kitaendelea kuheshimiwa huko Signal Iduna Park.

Aubameyang, kwa sasa anaonekana kuwa lulu kwenye kikosi cha Borussia Dortmund, kufuatia makali ya ushambuliaji anayoendelea kuyaonyesha msimu huu, ambapo mpaka sasa ameshafanikiwa kupachika mabnao 18 katika michezo 17 aliyocheza.

Maalim Seif apigilia Msumari Rasmi Zanzibar, Apinga Kauli za CCM
Newcaste United Wamnyatia Jonjo Shelvey