Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA limeiomba serikali kuwapa mafao ambao walikuwa watumishi wa serikali na baadaye kuondolewa kwa kosa la kugushi vyeti ama kuwa na vyeti feki

Hayo yamesemwa na Rais wa shirikisho hilo, Tumaini Nyamhokya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa mbali na watumishi hao kuwa na makosa ya kutumia vyeti feki lakini ni watumishi ambao waliweza kulitumikia taifa kwa uaminifu

Amesema kuwa endapo kama kuna watumishi wa umma wana vyeti feki vinavyosomeka kama vya darasa la saba shirikisho litawachukuliwa hatua  kwa kuweka majina yao bayana na kuongeza kuwa waraka uliotolewa na wizara ya utumishi wa umma na utawala bora haujatoa ruhusa kwa wakurugenzi wa halmashauri na mashirika kuwaondoa kazini watumishi wenye vyeti feki vya darasa la saba.

Hata hivyo, Rais huyo wa TUCTA amefikia hatua hiyo mara baada ya zoezi la serikali kuanza kufanya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wote wa umma ambao wako serikalini ili

Waalimu wa kiume matatani Njombe
Magazeti ya Tanzania leo Agosti 20, 2017