Jeshi la Polisi mkoanii Mbeya limesema litawapandisha kizimbani Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga baada ya upepelezi wa tuhuma za uchochezi kukamilika.

Ambapo Sugu anatuhumiwa kutoa kauli ya kichochezi inayodai kuwa kuna watu wanauawa mchana kweupe na miili yao kuwekwa kwenye viroba na kutupwa baharini.

Sugu pia amesema mkuu wa mkoa wa Mbeya anamsaidia Naibu Spika kupata ubunge, na kuunga mkono kauli ya askofu Kakobe kuwa Rais Magufuli anapaswa kutubu kwa kudumaza uchumi wa nchi na kupelekea maisha magumu kwa Watanzania.

Aidha Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limesema kuwa upelelezi wa tuhuma hizo za uchochezi umekamilika na wao kwasasa wanasubiri maamuzi ya mahakama ambayo yatafikiwa hivi leo.

 

Lissu afunguka Lowassa kwenda Ikulu, ‘sio cha kunyamaziwa’
Mbowe apishana na kauli za Lowassa alipokuwa Ikulu