Watu sita wa kundi la Oath Keepers nchini Marekani wamefunguliwa mashtaka kwa kupanga uvamizi kwenye jengo la Bunge la nchi hiyo.

Kulingana na taarifa ya Wizara ya Sheria, wanachama hao wa kikundi cha Oath Keepers ambao ni Graydon Young, Kelly Meggs, Connie Meggs, Laura Steele, Sandra Parker na Bennie Parker, walituhumiwa  kupanga njama ya kutekeleza uvamizi kwenye jengo la Bunge mnamo Januari 6 mwaka huu.

Imeelezwa kuwa watu hao walikula ya njama  ya kuvamia na kupora mali za serikali ya Marekani na kuingia kwenye majengo ya umma kinyume cha sheria.

Awali, Idara ya Upelelezi ya Marekani (FBI) ilitangaza mwezi uliopita kwamba mkuu wa “Oath Keepers”, Thomas Edward Caldwell, mwenye umri wa miaka 65, Jessica Watkins na Donovan Ray Crowl walipanga uvamizi huo Januari 6.

Kaze amkingia kifua Sarpong
Pitso Mosimane: Tupo tayari kwa mchezo, hakuna la kuhofia