Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, amemuumbua Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla baada ya kukanusha taarifa ya bohari za dawa kuwa haziko chini ya kiwango.
Aidha, Naibu Spika amelazimika kutoa maelekezo kwa serikali kuangalia Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) juu ya ubovu wa bohari za dawa nchini na kuzifanyia kazi kasoro kama watazikuta.
Hatua hiyo ya Dkt. Tulia imetokana na Dkt. Kigwangalla kukanusha taarifa ya bohari za dawa kuwa chini ya kiwango zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Halima Ally Mohamed.
Mbunge huyo akiuliza swali la nyongeza, amesema kwa mujibu wa taarifa ya CAG ya mwaka 2014/15, kuna bohari zisizo na viwango na kutaka kujua msimamo wa serikali ili kuhakikisha afya za Watanzania.
” Kwanza, naomba nikanushe vikali sana kwamba kuna bohari za dawa zisizo na viwango, hiyo ni ripoti ya CAG na hii ni taarifa ya Serikali, kwa hiyo naongea kama serikali kwa mamlaka kamili niliyopewa.”amesema Kigwangalla
Amesema bohari zilizopo ni za viwango vya hali ya juu na vimethibitishwa na Shirika la Kimataifa la Viwango (ISO), na zinakaguliwa kila baada ya miaka mitano na dawa haziwezi kutunzwa kwenye bohari zisizo na viwango kwa sababu zitaharibika.
Hata hivyo, Kufuatia majibu hayo Dkt. Tulia amesema kwa kuwa mbunge huyo ameuliza taarifa zinazotokana na Ripoti ya CAG, Serikali iangalie katika hiyo ripoti inasema nini ili kama alichosema mbunge kipo sawa ama hakipo sawa.

Philipp Lahm Atangaza Kustaafu Soka
Msukuma apingana na Makonda, ataka mali zake zichunguzwe