Dkt. Tulia Ackson ameongoza katika kura za maoni katika Jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya CCM kwa kupigiwa kura 843 akifuatiwa na mshindi wa pili Mahenge Mabula aliyepata kura 16 na mshindi wa tatu akiwa ni Charles Mwakipesile aliyepata kura 11.

Upande wa Ilala, aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo na Waziri wa Muungano na Mazingira, Mussa Zungu amepita kuwa kura 148, akiwapita Sophia Mjema aliyepata kura 105, Henry Sato, Massaba 4, Rahma Ngassa 6, Grace Buberwa 6.

Mtwara Mjini, Hawa Ghasia ameongoza kwa kura 440, Ruvuma Jenista Mhagama ameongoza kwa kura 854, Pangani amepita Juma Aweso kwa kura 282 huku Bukombe Dotto Biteko akiongoza kwa kura 555.

Dkt. Ndugulile aongoza kura za maoni Kigamboni, ampiku Makonda
Jafo, Lukuvi, Bashe waibuka kidedea kura za maoni