Watu wawili wakazi wa vijiji vya Nyamburi na Masongo mkoani Mara wamehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kila mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kumkeketa msichana mwenye umri wa miaka 14.

Wawili hao waliotajwa kwa jina la Wegesa John (60) mkazi wa kijiji cha Nyamburi na Mbusiro Ketari (53) kutoka kijiji cha Mosongo walihukumiwa kifungo hicho na Hakimu Mkazi, Amaria Mushi baada ya kukiri kutekeleza hali hiyo.

Wakiwa nje ya mahakama hiyo, Wawili hao ambao waliwalisikika wakidai kuwa walidanganywa kuwa Serikali imehalalisha ukeketaji.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Paskael Nkenyenge aliiambia Mahakama hiyo kuwa John na Mbusiro walitekeleza ukeketaji Desemba 15 mwaka huu na kukamatwa Desemba 16.

Watu hao hawakuelewa kama tayari wameshahukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela hata walipotoka mahakamani, hadi walipojikuta wakiwa chini ya ulinzi tayari kwa kupelekwa gerezani.

Akisoma hukumu hiyo mbele yao, Hakimu Mushi alisema kuwa kitendo cha ukeketaji ni cha kikatili na kinyume cha sheria, hivyo adhabu hiyo iwe fundisho kwa wengine.

Kaburi la Faru John ‘Hola..!’
Polepole atangaza 'vua gamba' ya CCM kivingine