Uongozi wa klabu ya Yanga umezungumza kwa mara ya kwanza kufuatia kuondoka kwa mlinzi wake kisiki, Gadiel Michael ambaye ametimkia kwa mahasimu wao timu ya Simba.

Gadiel Michael ametambulishwa na klabu ya Simba kuwa mchezaji wake rasmi kwa mkataba wa miaka miwili.

Aidha, uongozi wa Yanga kupitia kwa Meneja wake, Hafidh Saleh umesema kuwa wao kama klabu wameshamsahau Gadiel kwakuwa wameshasajili wachezaji bora kuliko yeye kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara.

“Gadiel Michael alikuwa mchezaji wetu, amemaliza kandarasi yake na hakupenda kuongeza mkataba ameamua kuondoka, kwahiyo kuna maisha mengine. Sisi tumeshamsahau ni kama historia kwetu kwasababu tumesajili majembe kuliko yeye,” amesema Hafidh Saleh.

Pia Hafidh amezungumzia maandalizi kamili ya kikosi cha Yanga kuelekea ufunguzi wa ligi mwishoni mwa mwezi ujao, ambapo amesema kuwa kikosi kamili pamoja na kocha Zahera watawasili wiki ijayo.

Huyu waziri ajiandae kutumbuliwa- Dkt. Bashiru Ally
Msaidizi wa Membe apatikana, ' Watekaji waliniuliza tukushushe wapi ambapo ni salama?