Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameitaka  Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kutomrudisha mgonjwa yeyote wa Saratani nyumbani kwa kukosa pesa ya matibabu.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akizindua bodi ya udhamini ya Taasisi hiyo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

“Mgonjwa anayefika kwenye Hospitali anatakiwa kupewa matibabu kwanza kisha tutaona namna ya kufanya lalini si kumrudisha nyimbani,” amesema.

Amesema, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inatekeleza azma yake kwa vitendo na inatatua changamoto za wananchi kwa kuhakikisha huduma bora zinatolewa nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Ummy ameahidi kuipatia Taasisi hiyo kiasi cha Shilingi bilioni 1.8 kwa ajili ya kununua mashine ya CT-SCAN itakayosaidia kuboresha huduma za matibabu.

Zoran Maki Kocha mpya Simba SC
Majaliwa 'awafunda' Mameya, Wenyeviti  Halmashauri