Tume ya taifa ya kutetea haki za kibinadamu nchini Kenya, KHCHR imedai kuwa jeshi la polisi nchini humo liliwaua watu 35 wakati wa ghasia zilizozuka wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti, Idadi hiyo ikiwa ni kubwa kuliko ilivyoripotiwa na mashirika mengine ya haki za kibinadamu.

Mwishoni mwa mwezi Agosti, shirika la Human Rights Watch lilisema watu 12 waliuawa na wengine 100 kujeruhiwa polisi walipokuwa wakikabiliana na waandamanaji maeneo ya magharibi mwa Kenya.

Shirika hilo halikutoa idadi ya waliofariki jijini Nairobi na miji mingine wakati huo lakini shirika la KNHCR imesema ni watu wawili pekee kati ya 37 waliofariki wakati huo ambao hawakuuawa na polisi.

Ikizindua ripoti kuhusu uchaguzi huo Jumatatu jijini Nairobi, KNCHR imesema kuwa polisi pia walitumia nguvu kupita kiasi katika kukabiliana na waandamanji wa mrengo wa upinzani National Super Alliance (Nasa) walipokuwa wakiwatawanya.

Mbali na kuripolti mauaji yaliyotokea ripoti hiyo iliyoandaliwa baada ya kufuatilia uchaguzi pia imedai kuwepo kwa uvunjaji wa sheria za uchaguzi kwa wanasiasa waliokuwa wakiwania nyadhifa mbalimbali.

KNCHR inadai kuwa mbali na kuwepo visa vya utoaji hongo kwa wapiga kura kulitokea pia usafirishaji wa wapiga kura kuelekea maeneo fulani na kuwepo kwa vifaa vya kampeni katika vituo vya kupigia kura kinyume na sheria.

Vurugu kubwa zilitokea kati ya waandamanaji wa upinzani na polisi yalizuka kati ya tarehe 9 na 15 mwezi Agosti baada ya tume huru inayosimamia uchaguzi nchini, IEBC, kumtangaza Rais wa sasa Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais.

IGP Sirro aagiza wafanyabiashara wakamatwe
Rais Karia apongeza baraza jipya la mawaziri