Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Corneille Nangaa, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia mawasiliano ya Satellite kuwa Congo ina njia mbili za kukubali matokeo hayo au kuyafuta.

Amesema kuwa iwapo matokeo yatafutwa, nchi haitakuwa na rais mpya mpaka uchaguzi mwingine utakapo anadaliwa.

Aidha, baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa kiti cha urais, ambapo Felix Tshisekedi aliibuka kidedea, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana New York Ijumaa kuzungumzia uchaguzi huo.

Rais aliyeko madarakani, Joseph Kabila tayari ameendelea kutawala kwa zaidi ya miaka miwili baada ya muhula wake kumalizika, na alikuwa tayari amejitayarisha kuachia madaraka mwezi huu mara tu rais mpya atakapo chaguliwa.

Hata hivyo, katika uchaguzi huo, Kabila alimuunga mkono waziri wake wa mambo ya ndani wa zamani, Emmanuel Shadary, ambaye alichukuwa nafasi ya tatu, huku wafuasi wa Fayulu wakimtuhumu Kabila kwa kufanya makubaliano na tume ya uchaguzi kumnyima mgombea wao ushindi wa urais.

DRC haijawahi kubadilishana madaraka kwa njia ya amani tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji mwaka 1960.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 12, 2019
Wahandisi wa maji wakalia kuti kavu