Mgombea wa Urais-Jean Pierre Bemba amesema kuwa uchaguzi umecheleweshwa kwa makusudi na mahakama ya kikatiba nchini humo ili kuweza kumnyima haki yake ya kimsingi ya kugombea nafasi hiyo ya Uraisi.

Bemba ambaye ni miongoni mwa wagombea 6 walioondolewa kwenye orodha ya kugombania urais na tume ya uchaguzi kwenye zoezi hilo lililopangwa kufanyika Disemba 23.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, wakati akifanya mahojiano na televisheni ya France 24, Bemba amesema kuwa ni jambo la kuhuzunisha kumuona rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akichagua ni nani watakaokuwa wapinzani wake.

Aidha, Rais Joseph Kabila ambaye ametawala taifa hilo tangu 2001 alitangaza kutowania urais kwa muhula mwingine baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.

Hata hivyo, hali ya taharuki na ghasia imeendelea kushuhudiwa kote nchini humo. taifa hilo lililokuwa chini ya ukoloni wa Ubelgiji halijashuhudia mabadilishano ya amani ya madaraka tangu lilipojipatia uhuru mwaka wa 1960.

Video: Pigo la mwisho kwa Makonda, JPM afurahia kichaa cha Waziri Mpina, Dkt. Bashiru usiyemjua
Adam Lallana amfuata Raheem Sterling