Tume Huru ya Uchaguzi ya Kenya (IEBC) imejibu madai ya kambi ya muungano wa NASA kuwa wapiga kura ambao tayari ni marehemu bado wako kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Kupitia taarifa yake kwa umma, Tume hiyo imesema kuwa imewathibitisha wapiga kura milioni 19.6 wenye sifa watakaoshiriki katika uchaguzi mkuu wa Agosti 8 mwaka huu, na kwamba uthibitisho wa wapiga kura hao ulifanywa kwa ushirikiano wa kampuni ya kufanya ukaguzi ya KPMG.

IEBC imeeleza kuwa kutokana na ukaguzi uliofanywa na KPMG, jumla ya majina 88,602 yaliyothibitishwa kuwa ni ya marehemu yaliondolewa kwenye orodha ya watakaopiga kura. Imeongeza kuwa ili kuhakikisha upigaji kuwa unakuwa na ufanisi, katika siku ya kupiga kura mfumo wa kielektroniki (biometric) utatumika kuwathibitisha wapiga kura.

Jana, NASA waliitaka Tume hiyo kuitisha mkutano wa dharura na vyama vya siasa wakidai kuwa uthibitishaji wa majina ya wapiga kura kwenye daftari la kudumu uliofanywa na IEBC hivi karibuni ulikuwa na mapungufu.

Utafiti: Kenyatta kumshinda Odinga uchaguzi Kenya
Diamond asema 'neno' kuhusu agizo la Rais kwa wanafunzi watakaopata mimba