Tume ya Uchaguzi Nchini Kenya (IEBC) imeingia lawamani mara baada ya kugawa tenda ya utengenezaji wa karatasi za kupigia kura yenye thamani ya shil. bilioni 2.5 kwa Kampuni ya Al Gurair ya Dubai, kitu ambacho kimewafanya vyama vya upinzani kutoa shinikizo kwa tume hiyo ya uchaguzi kusitisha tenda mara moja.

Aidha, suala hilo limekuja wakati tume hiyo ikifanya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika Agosti 8 mwaka huu.

Kwa upande wa vyama vya upinzani nchini humo vimepinga hatua hiyo ya kupewa tenda kwa Kampuni hiyo kwani inatiliwa mashaka makubwa ya kuwepo kwa harufu ya ufisadi.

“Kuna mawakala wanapigania tenda huko nje, lakini Tume haiwezi kuruhusu vita za mawakala na watu binafsi waharibu mchakato wetu wa uchaguzi mkuu, ndio maana tunafuta tenda zote,” amesema Mwenyekithi wa Tume hiyo Wafula Chebukati.

Hata hivyo, Uchaguzi Mkuu Nchini Kenya uanatarajiwa kufanyika Agosti 8 mwaka huu huku kukiwa na mvutano mkubwa katika kampeni hizo.

 

Mbunge wa Kibaha awakumbuka wananchi wake
Wananchi watahadharishwa kuhusu ugonjwa wa Nguruwe