Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema  Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli imetoa  kipaumbele kikubwa katika kuboresha sekta ya elimu nchini, na hayo yamemejidhihirisha kwenye bajeti ya mwaka 2016/2017 ambapo Serikali imetenga sh. trilioni 1.3 kwa ajili ya Sekta hiyo.

Majaliwa amesema kwenye harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya uboreshaji wa shule nchini iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Saalam.

Amewahakikishia wananchi kwamba bajeti ya Sekta ya elimu itaendelea kuongezeka kadri uwezo wa Serikali utakavyokuwa unaimarika.

“Kama mnavyofahamu, Serikali iliamua kuanza mara moja, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 ambayo inaelekeza Serikali kutoa elimu bure kwa watanzania wote kuanzia shule ya Msingi hadi Sekondari,” – Majaliwa.

Majaliwa pia alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi na wananchi wa Mikoa hiyo kwa kushiriki kikamilifu katika kumaliza kadhia hiyo kwa wanafunzi ambao walikuwa wanakaa chini. “Huo ndio uongozi tunaoutaka, uongozi wa kusimama bega kwa bega na wananchi na kutatua kero zao”,.

 

#HapoKale
Lowassa awafungukia wanasiasa waliodai ni ‘mgonjwa atakufa’