Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Taifa, Fortunatus Muslim amesema kuwa zoezi linaloendelea nchini la kukagua leseni, linazingatia sheria ya udereva ya mwaka 1965 ambayo inatoa mamlaka ya kukagua aina yoyote ya chombo cha usafiri.

Amesema kuwa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani halikagui vyeti bali ni leseni kutokana na sheria ya udereva ya mwaka 1965 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 1996, hivyo kuwataka wananchi kuondoa hofu.

“Dereva wa gari yoyote, wewe jiandae tu na leseni yako, pamoja na vielelezo kamili ili tujue leseni uliipataje, wala hatuna shida na mtu sisi tunahitaji kuhakiki tu, punguzeni presha za mitandaoni, hatukagui vyeti sisi,”amesema Kamanda Muslim

Aidha, ameongeza kuwa utaratibu wa kupata leseni ni kuanza masomo chuoni kwa miezi mitatu na baada ya kutahiniwa na polisi kisha TRA ambao wanatoa leseni, na kwa kuuwisha (renew) ni baada ya miaka mitatu na dereva lazima aingie darasani kwa mafunzo kila anapotaka kuongeza daraja.

Hata hivyo, Kamanda Musilim ameongeza kuwa kila dereva atapaswa kuwa na cheti kwa mujibu wa Mamlaka ya mafunzo ya ufundi stadi (VETA) kulingana na sheria ya bunge mwaka 2006, na cheti hicho kinapaswa kutolewa na vyuo ambavyo vimesajiliwa kwa ithibati toka (VETA)

Arsenal yamuweka njia panda Aaron Ramsey
Video: Maendeleo si kutukanana- Polepole