Rais Samia Suluhu Hassan amewataka mawaziri Vijana na Viongozi wanaotumikia wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kuleta matokeo ya haraka kwa miradi inayosaidia maendeleo ya jamii.

Rais Samia Suluhu ameyasema hayo leo tarehe 17 Oktoba alipotembela kituo cha kusukuma maji namba 5 Chekereni jijini Arusha.

Katika mazungumzo yake, Rais Samia amemsifu Waziri wa Maji Jumaa Aweso kwa uchapakazi na utendaji unaoleta matunda chanya kwa jamii.

“Hawa mawaziri kama Aweso ni vijana wachapakazi hatutumbui, ila mkisikia tunatumbua ni wale legelege” Amesema Rais Samia.

Rais Samia ameongeza kuwa Changamoto ya maji kwa mkoa wa Arusha imeshafanyiwa kazi na kuhusu barabara Serikali itakaa na viongozi wa Mkoa na wilaya zote za Arusha kujua barabara za kipaumbele ambazo zinatakiwa kuanza kushughulikiwa.

Awali akitoa Shukrani zake kwa Rais Samia, Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema kwa kipindi cha miezi 6 viongozi vijana wamemuelewa Rais na utendaji wake huku akishukuru kwa ushirikiano serikali inaoutoa kwa wizara ya maji kuhakikisha wananchi wa vijijini na mijini wanapata maji safi na salama.

Mradi huo umegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni usambazaji wa maji safi, huduma ya ugawaji wa majitaka na Kujenga uwezo wa Taasisi wa jiji la Arusha, ambao unatarajiwa kukabidhiwa kwa Mkoa wa Arusha mwaka mezi wa 6.

Kutumia picha za kughushi ni kosa kisheria:Serikali
Wananchi Sudan wapinga Serikali ya mpito