Shirikisho la soka nchini (TFF), limetangaza ujio wa mashindano ya Kombe la Soka la Ufukweni ambalo litafahamika rasmi kwa jina la Copa Dar es Salaam.

Shindano la kuwania Copa Dar es Salaam, limepangwa kufanyika Desemba 25 na 26, mwaka huu kwenye Uwanja/Ufukwe Coco ulioko Oysterbay, Dar es Salaam.

Tayari TFF imezialika timu za Zanzibar, Malawi na Uganda kushiriki michuano hiyo maalumu ya siku mbili. Timu waalikwa zimepewa hadi Desemba 12, mwaka huu kuthibitisha ushiriki wao.

Malengo ya michuano hiyo mbali ya kujenga na kudumisha urafiki baina ya nchi husika ambazo ni sehemu ya nchi majirani, madhumuni mengine ni kuboresha uwezo wa timu za taifa husika kabla ya kuanza kushiriki michuano mbalimbali ya kimataifa.

Mashindano hayo yamekuja wakati mwafaka hapa Tanzania kwani yatafanyika mara baada ya TFF kuendesha ligi ya makundi ya soka la ufukweni kwa timu za vyuo vya elimu ya juu ambayo sasa yamefikia hatua ya robo fainali.

Mechi za Robo Fainali ya ligi hiyo; Nusu Fainali, Mshindi wa Tatu na Fainali yenyewe zitachezwa Desemba 23, mwaka huu ikiwa ni siku mbili kabla ya kufanyika Copa Dar es Salaam inayoanza Desemba 25.

Katika hatua za robo fainali ni Chuo cha DIT kitacheza na AMCET wakati IFM itapambana na Herbert Kairuki huku Ardhi ikichuana na CBE vilevile TIA itavutana na DSJ.

TFF yamlilia Joel Nkaya Bendera
Harmonize, Sarah uso kwa uso na Wolper usiku wa leo