Mba kichwani kwa watu wanaosuka limekuwa ni tatizo ambalo linawasumbuwa wengi, kumekuwa na dawa za kisasa za kuondoa mba lakini pia kumekuwa na dawa za asili ambapo mimea na matunda hutumika.

Limao ni moja ya matunda yanayoweza kuondoa mba kichwani, unaweza kukabiliana na tatizo hilo kwa kuchukua maganda ya limao manne hadi matano na maji vikombe vinne kisha chemsha kwa moto wa kiasi kwa dakika 10 hadi 15.

Ambapo maji yakishachemka hadi kubadili rangi unashauriwa uyaache yapoe kisha osha nywele zako na kuhakikisha maji yamefika hadi kwenye ngozi ya kichwa.

Mganda haya ya limao husaidia kupunguza uwezekano wa kupata mba na pia kuacha nywele zikiwa zinanukia vizuri.

Matumizi ya maganda ya limao husidia ukuaji wa nywele zako, lakini pia huacha ngozi ya kichwa ikiwa laini na isiyo pauka.

 

LIVE IKULU: Rais Magufuli akiwaapisha viongozi mbali mbali aliowateua hivi karibuni
Athari za kulala mchana kwa binadamu