Baada ya kukaa mahabusu kwa siku nne, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema kuwa maneno anayoshtakiwa kwa kuyatamka ni ya kweli na kuwa siyo kosa.
Lissu ambaye yupo nje kwa dhamana, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka manne ya kutoa maneno ya uchochezi na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa.
Awali, kabla ya kupandishwa kizimbani mbunge huyo aligoma kula akiwa mahabusu ya polisi kwa mujibu wa wakili wake, Peter Kibatala.
Kutoka kwa Lissu kumefuatia kasoro za kuandaa kiapo kuwa mojawapo wa sababu zilizoifanya Mahakama hiyo kutupa pingamizi la dhamana lililowekwa na upande wa Serikali.
Aidha Mbunge huyo amepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka manne ya kutoa kauli za uchochezi, ambapo upande wa mashtaka uliwasilisha ombi la zuio la dhamana lililoambatana na kiapo cha Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Wilaya Ilala, Mrakabu Msaidizi (ASP), Denis Mjumba.
Vile vile, mahakama hiyo imetupa pingamizi la dhamana pamoja na mambo mengine kutokana na kasoro katika kiapo hicho.
Akitoa uamuzi wa pingamizi hilo, Hakimu Mkazi, Huruma Shaidi ameainisha mambo matatu yaliyomfanya kulikataa pingamizi hilo na kuamua kumwachia kwa dhamana mtuhumiwa.
Hata hivyo, Lissu ametimiza masharti hayo na kudhaminiwa na Diwani wa Kata ya Tabata wa chama hicho, Patrick Asenga hivyo akaachiwa huru

Camaroon, Misri Zapanda Viwango Vya Ubora Wa Soka
Viongozi wa dini wamuunga mkono Makonda kuhusu dawa za kulevya