Siku moja baada ya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kujisalimisha katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka ya uchochezi na kisha kuachiwa kwa dhamana, mbunge huyo amenasa tena kwenye mikono ya polisi.

Leo, Tundu Lissu alihojiwa tena kwa saa tatu na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutoa kauli nyingine za kichochezi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana nje ya mahakama ya Kisutu.

Hata hivyo, Lissu alilazimika kulala rumande baada ya kushindwa kukamilisha taratibu za dhamana.

Ingawa Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam hakuweza kulizungumzia tukio hilo kutokana na kuwa na shughuli nyingine za kikazi, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alithibitisha kuwa Lissu atalala rumande leo baada ya kukosa dhamana.

Lissu anakabiriwa na mashtaka ya uchochezi kwa kile alichokiandika kwenye mitandao ya kijamii na kuhusika katika chapisho moja kwenye gazeti la Mawio ambalo lilifutwa na serikali. Lissu na mhariri wa gazeti hilo jana walikana mashtaka ya uchochezi dhidi yao.

Ajabu: Mwanaume afunga ndoa na ‘simu yake’ kanisani
Wanamgambo 4 Wauawa na Jeshi la Kenya Lamu