Mbunge wa Singida Mashariki ambaye sasa yupo Kenya akiendelea na matibabu kufuatia tukio lake la kupigwa risasi lililotokea Septemba 7, 2017 amefunguka juu ya tabia iliyozuka kwa baadhi ya viongozi wa Chadema wanaokisaliti chama na kuhamia chama pinzani.

Lissu amefunguka kwa  kuwatia moyo viongozi waliopo ndani ya chama hicho kwa kusema jambo hilo lisiwatishe bali wao waendelee na kazi yao, kwani hata hao waliokisaliti chama hawajawahi kuwa na mafanaikio katika maisha yao.

Tundu Lissu ameyasema hayo pindi alipoonana na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Taifa, Patrick Ole Sosopi ambaye alimtembelea Mhe Lissu hospitali jijini Nairobi jana kumjulia hali.

‘’Hali ya siasa yetu ndani ya nchi yetu kwa biashara inayoendelea kununua Viongozi uchwara na wenye tamaa wa chama chetu, amesema mbona Yesu aliwahi kusalitiwa tena na mwanafunzi wake, tusipate hofu Chadema hatujaanza kusalitiwa leo na hao wanaondoka, sio ajabu hata kidogo kazi yake, Yesua lisalitiw ana wanafunzi wake na hakuacha kazi hata kidogo” ameandika Ole Sosopi ujumbe kutoka kwa Tundu Lissu.

Ameendelea kwa kusema “Wanaotusaliti hawajawahi kuwa na mafanikio katika maisha yao, tusikate tamaa mapambano yaendelee.

Aidha Lissu amewaomba Watanzania wanaoendelea Kumchangia na Kumuombea,

 

 

.

 

Atiwa mbaroni kwa kuuza watoto pacha
JPM amwaga mapesa mkutano wa CWT