Baraza la vijana Chadema wametakiwa kuwa mstari wa kwanza kudai haki na kutetea upatikanaji wa katiba ya wananchi ili iweze kutumika katika uchaguzi mkuu ujao

Akizungumza na vijana hao hivi karibuni aliyekuwa mwenyekiti wa CCM na Swahiba wa karibu sana na Mh. Edward Lowassa Bw. Hamis Mngeja amewaambia vijana hao pasipo kupigania upatikanaji wa katiba mpya ya wananchi ni sawa na kufanya kazi bila malipo.

”Niwaambie ukweli ili tushinde vita hii ya kushinda kwa uhalali lazima tupate katiba mpya, lakini tusikubali kwenda na katiba hii iliyopo kwenye uchaguzi mkuu ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu”. alisema Mngeja.

Aidha Mngeja amesema kwamba vijana ni chachu ya mabadiliko ndani ya jamii na chama kwa ujumla hivyo wasikate tamaa hata wanapobezwa kwani mafanikio ya kazi wanazozifanya yapo njiani.

Pamoja na hayo Mngeja ameitaka serikali kuacha kunyima uhuru wananchi wake kwa kuweka sheria ambazo zinabana ikiwepo hili la tamko la kuzuia mikutano ya kisiasa mpaka 2020.

”Kwani sisi tukifanya mikutano tunashika mafaili ya Makonda au Majaliwa? tusinyimane uhuru kwani hakuna mwenye nchi bali tunapeana dhamana” alisema Mngeja.

 

 

 

Joseph Omog Awakataa Wachezaji Wa Kigeni Simba SC
Magari Ya Kutumia Umeme Yaanza Kufanya Kazi Nchini Kenya