Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Hbari mwaka 2022 zimezinduliwa rasmi Mjini Bukoba Mkoani Kagera, zikiwa na makundi mawili mapya ya Habari za Sensa, Kodi, Tozo na Mapato.

Kwa mwaka huu (2022), kipengele cha Mchora Katuni Bora, Mpiga Picha bora wa Runinga na Mpiga Picha Bora wa Magazeti kimeondolewa katika kinyang’anyiro kutokana na mwitikio mdogo wa washiriki.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Nchini, MCT, Kajubi Mukajanga (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Kagera, Mbeki Mbeki.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga pia amezindua fomu ya kutuma kazi za waandishi kwa njia ya mtandao, zitakazowawezesha kushiriki wa Shindano hilo.

Fei Toto awaomba msaada mashabiki
Hersi Said: Tupo tayari kukabili Club Africain