Tuzo za 64 za Grammy zilizokuwa zikitarajiwa kufanyika januari 31 mwaka 2022, zimeahirishwa kutokana na kuongezeka kwa kesi za Covid-19 nchini Marekani.

Kwa mujibu wa waandaji wa tuzo hizo zenye heshima kubwa Duniani,  Siku ya Jumatano waliweka wazi kuwa tukio hilo litapangwa upya na tarehe yake itatangazwa rasmi mapema baada ya kujiridhisha na kupungua kwa kesi za kuenea kwa Covid-19.

“Baada ya kutafakari kwa kina na kuchambua kwa kushirikiana na maafisa wa jiji na serikali, wataalam wa afya na usalama, jumuiya ya wasanii na washirika wetu wengi, Recording academy na CBS wameahirisha onyesho la 64 la kila mwaka la utolewaji wa tuzo za GRAMMY.” taarifa hiyo ilisema.

“Afya na usalama wa wale walio katika jumuiya yetu ya muziki, hadhira ya moja kwa moja, na mamia ya watu wanaofanya kazi bila kuchoka ili kutuunga mkono inabakia kuwa kipaumbele chetu, kufanya onyesho mnamo Januari 31 pia kunajumuisha, hatari nyingi hivyo tuna ahirisha kwa muda.” Ilihitimisha taarifa hiyo.

Tuzo hizo zilipangwa kufanyika Los Angeles nchini Marekani, Siku ya Jumanne pekee, na watu takriban 21,790 katika Kaunti ya Los Angeles walipima virusi vya COVID-19.

Kulingana na ofisi ya Afya ya Umma ya LA County, na takriban watu 2,000 katika kaunti hiyo walilazwa hospitalini baada ya kukutwa na virusi hivyo, jambo lililozua hofu iliyopelekea kusimamishwa kwa tukio hilo.

Mchakato wa uteuzi wa washiriki wa tuzo hizo ulitangazwa mnamo Novemba 23 2021. Ambapo wasanii kadhaa walitajwa kuwania kwenye vinyang’anyiro mbali mbali.

Wasanii kama Justine bieber na H.E.R ni miongoni mwa wasanii wa waliotajwa zaidi kwenye vipengele takribani nane, huku rapa Jay z akiingia kwenye headlines baada ya kuwa msanii aliyeteuliwa zaidi katika historia ya onyesho hilo.

Wema Sepetu ashambuliwa kisa picha ya mtoto mchanga
Gwajima: Spika Ndugai ajiuzulu, kuna nia ovu