Chama cha wachezaji wa kulipwa nchini England (PFA) kimetoa orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa 2016/17.

Katika orodha hiyo vinara wa ligi ya nchini England (Chelsea) wana wachezaji wawili Eden Hazard na N’Golo Kante.

Wengine ni Zlatan Ibrahimovic(Manchester United), Harry Kane (Tottenham), Romelu Lukaku (Everton) na  Alexis Sanchez (Arsenal).

Orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora mwenye umri wa mdogo:

Dele Alli na Harry Kane – Tottenham Hotspur

Michael Keane – Burnley

Romelu Lukaku – Everton

Jordan Pickford – Sunderland

Leroy Sane – Manchester City

Orodha ya Wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa PFA upande wa wanawake:

Lucy Bronze – Manchester City Women

Karen Carney – Chelsea Ladies

Jane Ross – Manchester City Women

Jill Scott – Manchester City Women

Caroline Weir – Liverpool Ladies

Ellen White – Birmingham City Ladies

Orodha ya Wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka mwenye umri mdogo kwa wanawake:

Millie Bright – Chelsea Ladies

Jess Carter – Birmingham City Ladies

Nikita Parris – Manchester City Women

Georgia Stanway – Manchester City Women

Keira Walsh – Manchester City Women

Caroline Weir – Liverpool Ladies

Hafla ya kutangaza washindi wa tuzo ya PFA imepangwa kufanyika  Aprili 23.

Kiungo mshambuliaji wa Leicester City Riyad Mahrez na mshambuliaji wa kikosi cha wanawake cha Manchester City Izzy Christiansen  walitangazwa washindi wa tuzo ya PFA msimu uliopita sanjari na mshambuliaji kinda wa Sunderland Beth Mead (20), ambaye alitwaa tuzo ya mchezaji bora mwenye umri mdogo upande wa wanawake.

Dele Alli alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji mwenye umri mdogo upande wa wanaume msimu uliopita.

Vijana Wa Gabon Kuipima Serengeti Boys
Mbao FC Kumchunguza Erick Ngwengwe