Taasisi ya Utafiti Twaweza leo, Februari 27, 2018 imetoa matokeo ya utafiti uliohusisha watoto 197,451 katika shule za msingi 4750 yakidai kuwa 38% ya watoto wenye umri wa miaka 9 hadi 13 nchini hawawezi kufanya majaribio ya darasa la pili.

Matokeo hayo yametolewa na Mkurugenzi wa Twaweza, Aidan Eyakuze ambapo amesema usawa katika kujifunza ni changamoto nchini.

Ameeleza kwamba tofauti hizo zinaonyesha kwamba eneo analoishi mtoto lina mchango mkubwa katika kujifunza.

Aidha Eyakuze amesema kuwa 42% ya watoto kutoka kaya maskini walifaulu majaribio ikilinganishwa na 58% ya watoto kutoka kaya zenye uwezo.

Amesema kuwa matabaka haya yanajitokeza kwenye jamii hali ambayo ikiachwa iendelee inaweza kuwaacha maskini wakaendelea kuwa maskini.

Pia ameongezea kuwa familia zenye wazazi waliosoma kwa 74% watoto wao kwa kiwango kikubwa wamefanya vizuri katika majaribio haya ukilinganisha na watoto waliotoka kwenye familia ambazo hazijasoma.

Majaribio hayo yamefanywa kwenye somo la kusoma, kingereza na hesabu rahisi.

TANNA yalaani vikali shambulio kuuawa kwa muuguzi Bugando
Serikali kutoa chanjo ya saratani kwa watoto wa kike