Machi 29, 2018 Taasisi ya Twaweza imezindua ripoti yake ya Utafiti wa Sauti za Wananchi awamu ya 25, ambapo umeonesha kuwa taarifa zinazotolewa na rais zinaaminika kwa asilimia 70 huku zile zinazotolewa na Makamu wa rais zinaaminika kwa asilimia 64.

Ripoti hiyo imebainisha pia wabunge wa vyama vya upinzani taarifa zao huaminika kwa asilimia 12 pekee huku zile zinazotolewa na wabunge wa chama tawala yaani CCM huaminika kwa wananchi asilimia 26.

Kwa maana nyingine, asilimia 16 ya wananchi hawaamini kabisa taarifa zinazotolewa na wabunge wa upinzani huku asilimia 6 pekee ya wananchi hawaamini taarifa zinazotolewa na wabunge wa CCM.

Aidha ripoti hiyo pia imeonesha kuwa taarifa zinazotolewa na wanachama wa vyama vya upinzani zinaaminika kwa asilimia 9 ya wananchi huku wanachama wa chama tawala cha CCM taarifa zao zikiaminika kwa asilimia 27.

Kwa upande mwingine ripoti hiyo imeonesha kuwa taarifa zinazotolewa na wenyeviti wa mitaa na vijiji zinaaminika kwa asilimia 30 ya wananchi.

Viingilio mchezo wa Ngororngoro Heroes dhidi ya Congo DR vyatangazwa
Video: Yaliyojiri Mahakama ya Kisutu leo

Comments

comments