Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula amezitaka Halmashauri nchini kwenda na kasi ya Rais, Samia Suluhu Hassan kwa kutenga ardhi kwa ajili ya uwekezaji.

Dkt, Mabula, meyasema hayo wakati akihitimisha kikao kazi baina ya wakurugenzi wa Halmashauri na wataalamu wa sekta ya ardhi kikichofanyika jijini Dodoma.

Amesema, “Hata kama mmetenga maeneo je meyatwaa na ni ya kwenu au mkipata muwekezaji ndiyo mnaanza kuhangaika, hapa  kinachohitajika ni kwenda na kasi ya mhe rais na wakurugenzi  ndiyo ninyi na maafisa ardhi ndiyo ninyi.”

Sehemu ya washiriki wa kikao kazi kilichowaunganisha wakurugenzi wa Halmashauri na watalaam wa Sekta ya Ardhi nchini.

Akizungumzia suala la Halmashauri, juu ya kushikilia ardhi kwa muda mrefu bila kulipa fidia kwa wamiliki wake, Waziri amesema wanaposhindwa kulipa fidia ya eneo ililotwaa basi lirudishwe kwa muhusika na pale litakapohitajika ufanyike uthamini upya.

”Kuna ardhi mmezihold kwa miaka nenda rudi fidia hailipwi lakini mgogoro unakuja ardhi sasa tuseme ukishindwa kulipa fidia maana hiyo ardhi umrudishie mwenyewe ukitaka tena utafanya uthamini” amesema Dkt Mabula

Hata hivyo, Dkt Mabula, amefafanua kuwa, Serikali haitaki uonevu kwa wananchi kwa kuwa siyo maelekezo ya rais na kusisitiza kuwa serikali inathamini wawekezaji hata wa ndani na pale wanapokuja wawekezaji wa nje wale wa ndani wasionekani siyo lolote.

Zaidi ya Wanaume 500 waripotiwa kunyimwa unyumba, kupigwa
Nyerere day: Mashujaa wa Afrika na mafanikio ya AU