Hatimaye kikosi cha Timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ kimetinga hatua ya Fainali ya Michuano ya Ukanda wa Kusini mwa Afrika ‘2021 COSAFA Women’s Championship’.

Twiga Stars imekamilisha azma ya kucheza mchezo wa Fainali ya michuano hiyo, kufuatia kushinda mchezo wake wa Nusu Fainali dhidi ya Zambia, uliopigwa leo Alkhmis (Oktoba 07), kwenye Uwanja wa Nelson Mandela Bay mjini Port Elizabeth, Afrika Kusini.

Hadi dakika 90 za mchezo huo zinakamilika, timu hizo zilikua zimefungana bao 1-1, na ndipo sheria ya mikwaju wa Penati ilipochukua mkondo wake.
Katika hatua hiyo Twiga Stars ilipata mikwaju mitatu huku wapinznai wao Zambia wakipata mikwaju miwili, na kuifanya Tanzania kusonga mbele.

Twiga Stars itacheza mchezo wa Fainali na mshindi wa mchezo wa Nusu Fainali ya pili kati ya wenyeji Afrika Kusini dhidi ya Malawi.

TARURA rekebisheni mfumo wa maegesho ya Magari :RC Makala
Mtanzania ashinda Nobel