Kikosi cha timu ya Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa Amani na uwanja wa Mafunzo vilivyopo kisiwani Zanzibar.

 Twiga Stars iko kambini kisiwani Zanzibar kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) zitakazofanyika nchini Congo- Brazzavile kuanzia Septemba 04 – 19 mwaka huu.

Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage ameendelea kukinoa kikosi chake cha wachezaji 25 waliopo kambini kisiwani Zanzibar kujiandaa na michuano hiyo ya Afrika.

Twiga Stars itakua kambini kisiwani Zanzibar kwa kipindi cha mwezi mmoja, kujiandaa na fainali hizo za michezo ya afrika, ambapo imepangwa kundi A pamoja na wenyeji Congo – Brazzavile, Ivory Coast na Nigeria.

Dk. Slaa Kuongeza Nguvu Chadema, Lowassa Achukua Fomu Kwa Mafuriko
Basi La Hertha Berlin Lapigwa Risasi