Kikosi cha timu ya taifa ya Wanawake chini ya miaka 20, leo Ijumaa (Oktoba 22), kimefanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wa Mkondo wa Pili wa kuwania kufuzu Fainali za Afrika dhidi ya Namibia.

Mchezo huo utachezwa kesho Jumamosi (Oktoba 23) Uwanja wa Dobsonville, Soweto Afrika Kusini.

Kuelekea mchezo huo, Twiga Stars wana deni la kulipa, kufuatia kupoteza mpambano wa Mkondo wa Kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam Jumatano (Oktoba 20) Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Twiga Stars ilikubali kufungwa mabao 2-1, hali inayoifanya kusaka ushindi wa mabao 2-0 kwenye mpambano wa kesho Jumamosi (Oktoba 23) ili kujihakikishia nafasi kusonga mbele.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Twiga Stars.

Tanzania na Burundi kuimarisha mipaka
Manara afunguka tuzo za TFF