Mtandao wa Twitter umezifungia kwa muda akaunti za baadhi ya watu waliojihusisha na maandamano ya kutaka mabadiliko katika Kilimo nchini humo ikiwemo akaunti ya gazeti maarufu la Caravan linalowatetea Wakulima, Mwanaharakati Hansraj Meena na Mwigizaji Sushant Singh.

Hatua hiyo inatokana na ombi la kisheria lililopelekwa na Serikali kwa kigezo kuwa, machapisho katika akaunti hizo yanahatarisha usalama na utangamano wa India.

Mtandao huo wa kijamii umejitetea kufanya hivyo kutokana na kupokea agizo lenye Muhuri wa Mahakama.

Maelfu ya Wakulima nchini India wamekuwa wakiandamana tangu Novemba wakitaka Serikali ifanye mageuzi katika Sekta ya Kilimo.

Hussein Sleiman Ali kocha mpya Jang'ombe Boys
Himid Mao atua Entag El-Harby SC